Blog Details Home / Blog Details

Ziara Katika Kumbukumbu za Mwalimu Nyerere – Sehemu ya Makumbusho Butiama
Our history . 3rd Sep, 2025

Ziara Katika Kumbukumbu za Mwalimu Nyerere – Sehemu ya Makumbusho Butiama

Leo tarehe 3 Septemba 2025, wanafunzi na walimu walifanya ziara ya kihistoria katika Makumbusho ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yaliyopo Butiama, nyumbani kwa Baba wa Taifa. Ziara hii ilikuwa sehemu ya shughuli za maembeei, ikiwaleta pamoja viongozi, walimu na wanafunzi kwa lengo la kujifunza na kuenzi urithi wa historia ya taifa letu.

Katika ziara hiyo, washiriki walipata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali za makumbusho, ikiwemo:

  • Vyumba vya kumbukumbu binafsi za Mwalimu Nyerere.

  • Nyaraka na picha za kihistoria.

  • Sehemu alizopumzika na kufanya kazi za kitaifa.

  • Vifaa na zawadi mbalimbali alizopewa wakati wa uongozi wake.

Wageni wa heshima akiwemo Mkuu, Makamu, pamoja na walimu wengine walihudhuria tukio hili, likiwa alama ya mshikamano na hamasa kwa kizazi kipya kujifunza maadili ya uongozi, uzalendo na mshikamanano aliouacha Mwalimu Nyerere.

Kwa picha kamili za tukio hili adhimu, tembelea:
👉 Gallery ya picha

Ziara hii imeacha kumbukumbu ya pekee na kutufundisha thamani ya historia ya taifa letu, sambamba na kuhamasisha vijana kuishi kwa maadili na nidhamu ambayo Mwalimu aliyasimamia.

0 Comments

Leave A Comment

Sing in to post your comment or singup if you don’t have any account.